Klabu ya Real Madrid imezindua jezi tayari jezi mpya ambazo watazitumia kwenye msimu ujao wa soka katika mashindano tofauti kuanzia Ligi ya Mabingwa, Ligi Kuu ya Hispania na michuano mingine.
Jezi hiyo ambayo imetengenezwa na kampuni ya ADIDAS ambao ndio wadhamini wa mabingwa hawa mara 10 wa michuano ya Ulaya, imenakishiwa kwa rangi nyeupe ambayo ni rangi ya utamaduni ya Real Madrid huku ule weupe ukiwa unang’aa zaidi kuliko ilivyozoeleka kawaida.
Wachezaji wa Real Madrid akiwemo nahodha Iker Cassillas wameonekana wakiwa wamevalia jezi hii kwa mara ya kwanza wakiionyesha katika uzinduzi wake na tayari imeshainia sokoni tayari kuuzwa kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Uwepo wa Iker Cassilas kwenye matangazo ya jezi hizi umewachanganya wengi kutokana na taarifa zilizoenea kila mahali kuhusiana na nyota huyo kuwa yuko mbioni kuihama Real baada ya kuitumikia kwa muda mrefu kufuatia mipango ya klabu hiyo ya kumsajili kipa wa Manchester United, David De Gea.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.