Hii sio taarifa nzuri kwa fans wa Brazil baada ya staa wao Neymar kupunguzwa kenye Kikosi cha Timu hiyo.
Neymar amefungiwa mechi nne kutokana na utovu wa nidhamu Uwanjani ambapo alichukua mpira na kumpiga nao mgongoni Mchezaji wa Colombia, Pablo Armero ambapo katika mechi hiyo Brazil walifungwa 1-0.
Neymar alioneshwa kadi nyekundu na hukumu ya kwanza iliyotolewa ilikuwa Neymar akose mechi moja tu, lakini baadae Shirikisho la Soka Amerika Kusini walipitia upya kesi yake na kumwongezea adhabu na kumfungia mechi nne baada ya kugundua alitoa kauli mbaya kwa mwamuzi Enrique Osses.
Staa wa Colombia, Carlos Bacca nae kafungiwa kucheza mechi mbili lakini Shirikisho hilo limesema milango iko wazi kama jamaa wakiamua kukata rufaa.
https://www.youtube.com/watch?v=ZVxXChyaAV4
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.