Kama wengi tunavyojua mkali wa RnB Marekani Chris Brown ni baba mwenye mtoto mzuri wa kike aliempa jina la Royalty. Lakini Chris bwana amekua akitengeneza headlines zinazo wateka watu wengi kwenye Instagram baada ya kua ana post picha tofauti za yeye na mtoto wake pamoja.
Sawa, Chris Brown anaweza asiwe mtu mzuri sana kwenye mahusiano ya kimapenzi lakini utakubaliana na mimi kua jamaa anajitahidi kua baba bora kwa mtoto wake wa kike ambaye hivi juzi ametimiza mwaka mmoja. Emu zicheki hizi picha hapa chini mtu wangu ujione jinsi gani Chris anavyo onyesha upendo kwa mtoto wake wa kike Royalty, hadi raha yani! Yani kuanzia birthday ya mwanae, zawadi anazomletea, sehemu wanazoenda wote na hata wakiwa wamechill tu, zote hizi Chris anazitupia Instagram na kusababisha headlines mpya kwenye jina lake!
Wababa wanganpi uanowajua wana upendo huu watu wangu!?
Chris Brown alimnunulia mwanae hizi ndiga tatu, yani hapo ni kitu cha Lamborghini na Range Rover.
BAPE KINDA DAY! A photo posted by @chrisbrownofficial on
Akiwa anamlisha mwanae kipande cha nyama ya kuku. Ona hadi raha!
Happy Father’s Day to the real fathers. She changed my life. #GLAD2BEHERDAD A photo posted by @chrisbrownofficial on
Hapa Chris akiwa amechill na mwanae kwenye siku ya Fathers Day duniani.
Chris alipost ujumbe huu, comments alizozipata zilikua kutoka kwa mashabiki walioguswa na upendo wake!
@abielruiz thx for the wonderful painting for my daughter bro! A photo posted by @chrisbrownofficial on
Alimuita mchoraji nyumbani kwake ili amchoree mwane picha hii ya Mini Mick Mouse.
moja ya keki alizomtengenezea mwanae kwa ajili ya Birthday yake ya mwaka mmoja.
👑👑👑 A photo posted by @chrisbrownofficial on
Emu cheki mtu wangu, farasi akaletwa hadi nyumbani kwa ajili yake tu!
Hiki ni kipisi cha video kwenye siku ya Fathers Day duniani.
Chris Brown akampeleka mwanae Disney World kula good time kama baba na mwana.
Siku haikuweza kuisha bila picha ya pamoja ya Royalty, Micky na Minie Mouse huko Disney Land!
Hapa Chris Bown, Omarion na Tyga wote wakiwa pamoja wakila good time na watoto wao!
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.