Utajisikiaje pale unapopewa chakula kwenye ndege alafu unakutana na kitu ambacho hukukitegemea?
Ndani ya ndege ya Air India mmoja wa abiria kakutana na mjusi ndani ya Burger, safari ilianzia Delhi India kwenda London Uingereza..
Mhudumu wa ndege kamletea abiria Burger kama alivyoagiza bila kujua kwamba kuna kitu kingine ndani… abiria huyo alikasirika sana, lakini abiria wengine pia nao hawakupenda hii kitu, wakaamua kususa kula chakula chochote kilichogagiwa na wahudumu ndani ya ndege.
Ishu ilifika kwenye Uongozi baada ua kuchukua headlines nyingi mitandaoni, wao walikataa kwamba hakuna ukweli wowote!
Unahitaji chochote ninachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.