Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
kungekua na jimbo lenye wakinamama tupu tanzania wallahi ningetangaza nia….
— IMEBAKI STORY (@hemedyPHD) June 26, 2015
Ni muhimu sana kama taifa kukusanya nguvu kwa pamoja, tuwe na vision ya pamoja katika kuleta maendeleo ya taifa letu.
— Emmanuel Nchimbi (@nchimbie) June 26, 2015
Maendeleo ya kweli hayawezi kuletwa bila kusimamia utawala bora.
— Emmanuel Nchimbi (@nchimbie) June 26, 2015
Mahusiano na mataifa mengine kiuchumi yanawezesha wawekezaji kuweza kuwekeza nchini, na watanzania kufanya biashara na makampuni mengine.
— Emmanuel Nchimbi (@nchimbie) June 26, 2015
Uwekezaji makini wa wageni na wazawa ni njia ya moja kwa moja ya kupanua soko la ajira na soko la biashara
— Emmanuel Nchimbi (@nchimbie) June 26, 2015
Your favourite song #NaNa is Number two in Africa now… thanks alot for all who been supporting me and my… http://t.co/lZVktuP95U
— Diamond Platnumz (@diamondplatnumz) June 26, 2015
Naomba umoja, mshikamano na upendo utawale katika mchakato wa kumpata mgombea Urais kwa tiketi ya CCM. Sote tuendelee kuiombea nchi yetu
— Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) June 26, 2015
Blog
Mwananchi
Wagombea urais CCM wagonga 40
Mtafiti binafsi na kada wa CCM, Helena Elinawinga (41), amejitokeza kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama chake kuwania urais na kusema amefikia uamuzi huo ili kupunguza kujirudiarudia kwa adhabu za vifo kwa viongozi.
Helena anakuwa kada wa 40 wa CCM kuomba ridhaa ya chama hicho kuteuliwa kupeperusha bendera yake katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
=Kada huyo ni mwanamke wa sita kuchukua fomu za kuomba kuwania nafasi hiyo katika chama hicho akitanguliwa na Balozi Amina Salum Ali, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dk Mwele Malecela, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro, Monica Mbega na Ritta Ngowi.
Watoto waliwa na fisi, wafa
Watoto wawili wenye umri wa kati ya miaka miwili na mitano wameuawa na fisi katika Kijiji cha Mnkola, Kata ya Ibihwa wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma katika matukio mawili tofauti.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Teya Kata ya Ilindi wilayani hapa, Paul Mwaja alisema kuwa watoto hao wameuawa katika matukio mawili ndani ya kipindi cha wiki moja.
Mwaja alisema tukio la kwanza lilitokea juzi ambapo mtoto mmoja wa kiume mwenye aliuawa na fisi wakati akiwa na wenzie wawili wamelala. “Alikwenda fisi katika eneo hilo na kumvuta (mtoto mmoja) na kumtafuna hadi akamuua,”alisema Mwaja.
Tweet ya Obama :Leo tumepiga hatua kubwa kufikia lengo letu la kuwa haki sawa walio kwenye mahusiano ya kimapenzi ya jinsia moja sasa wana haki sawa za kufunga ndoa, kama vile ilivyo kwa watu wengine.
Habari Leo
Dk Shein kuvunja Baraza la Wawakilishi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein leo anahutubia Baraza la Wawakilishi, akitarajiwa kutumia fursa hiyo kuaga na kusitisha uhai wa Baraza hilo uliodumu kwa miaka mitano na hivyo kumaliza kazi yake kwa mujibu wa Katiba.
Hata hivyo, Makamu wake wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, amezuiwa kuingia baada ya wajumbe wa Baraza hilo kukataa kutoa kibali cha kumruhusu kuongozana na Dk Shein katika shughuli hiyo ya kuvunja baraza.
Maamuzi ya kumkataa Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambacho ni sehemu ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, yalifikiwa jana na wajumbe hao baada ya Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho kuwataka kuridhia kutolewa kibali kwa wageni atakaofuatana nao Dk Shein na kuingia nao ukumbi wa Baraza.
Mwanasport
SIMBA ipo katika hatua nzuri za kusajili kifaa kipya cha nane kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.
Mchezaji huyo ni straika Danny Lyanga ambaye amekuwa akihitajika na Yanga kila mara na kuidengulia kwa madai kwamba akili zake hazipo kwenye soka la Bongo.
Lyanga kwa sasa anaichezea FC Lupopo ya DR Congo ingawa hana mkataba nayo kwa madai kwamba mambo yao mengi yamekuwa magumashi na hawataki kumpa hela ya kueleweka, hivyo yuko katika mikakati ya kurudi kucheza soka nchini ndiyo maana Simba wakamwibukia fasta.
Endapo Simba watafanikiwa kupata saini ya Lyanga aliyewahi kung’ara na Coastal Union, basi atakuwa ni mchezaji wa nane katika usajili mpya unaowajumuisha Mussa Hassan ‘Mgosi’, Peter Mwalyanzi, Mohamed Fakhi, Samir Nuhu, Laudit Mavugo, Emery Nimubona pamoja na kipa wa JKU, Mohamed Abdulrahman ambaye bado hakijaeleweka kutokana na kubanwa wa mkataba wake uliobakiza mwaka mmoja na klabu yake.
Saleh Jembe
KOCHA MPYA SIMBA ATUA DAR, ASEMA ATAPAMBANA KUTENGENEZA SIMBA BORA
Kocha mpya wa Simba, Dylan Kerr amewasili jijini Dar es Salaam amesema atapambana kuhakikisha Simba inafanya vema.
Kerr raia wa Uingereza amewasili jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Simba, Collins Frisch.
“Sijui vitu vingi kuhusiana na soka la Tanzania lakini lengo ni kutengeneza kikosi bora chenye kuleta ushindi.
“Kwa sasa inaweza kuwa mapema sana kuzungumzia mambo mengi, lakini najua tutafanikiwa tukishirikiana.
“Simba ni timu kubwa na maarufu, hivyo ushirikiano utakuwa nguzo ya kufikia mafanikio,” alisema.
Kocha huyo anachukua nafasi ya Goran Kopunovic raia wa Serbia ambaye Simba iliamua kuachana naye baada ya kutaka Sh milioni 100 ili asaini mkataba wa miaka miwili.
Jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.