Kesi za majina ya wasanii kutumika kutapeli kupitia mitandao ya kijamii imeendelea kuchukua headlines kila wakati… Kwenye list ya Mastaa ambao waliwahi kukutana na ishu za aina hii yumo Flavian Matata, Young Dee na Izzo Business.
Soudy Brown leo yuko na Nikki wa Pili, moja ya members wa Crew ya Weusi, ishu ni kwamba kumbe account yenye jina la Joh Makini imetumika kutapeli baadhi ya wafanyabiashara kutoka Mikoani.
Wafanyabiashara wawili wamelalamika kutapeliwa na mtu ambaye katumia jina la Joh Makini, mmoja wao kamwamini kabisa kamtumia na pesa bila kujua kwamba anayewasiliana nae sio Joh Makini na wala hiyo account sio yake !!
Nikki Wa Pili ameongea na Soudy, amesema ni kweli amepigiwa simu na watu wakilalamika kutapeliwa hela ambazo waliahidiwa kutumiwa T-shirt za Weusi.. Nikki amesema watu hao waliwasiliana na matapeli wakitumia jina la Joh Makini.
U Heard niko nayo hapa pia mtu wangu, kama imekupita unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie