Stori ninayotaka kukusogezea sasa hivi ni hii kuhusu vijana wawili kutokea Tanzania (Given Edward & Angel Benedicto) ambao wiki iliyopita walikabidhiwa tuzo na malkia wa Uingereza kutokana na kile walichokifanya kwa jitihada zao.
Vijana walioteuliwa kuwania tuzo hizo za malkia wa Uingereza walikuwa 60 kati ya mamia ya washiriki na dhumuni kubwa ni kuwapongeza kwa mchango wao mkubwa wa kimaendelea katika nchi zao.
Akizungumza na waandishi wa habari leo July 1, 2015 Given Edward ambaye alikabidhiwa tuzo na malkia wa Uingereza alisema..’Kuna rafiki yangu mmoja aliona shughuli ninazofanya akaniambia kuwa kuna tuzo zinatolewa na malkia na anaamini kuwa naweza kupata kutokana na kushughulia ninayoifanya’
‘Walihitaji interview ambazo niliwahi kufanya na waandishi mbalimbali wakazihitaji kuhusu project zangu na wakataka na makampuni niliyowahi kufanya nayo kazi baada ya hapo basi wakatutangaza’
Sasa hivi itakuwa ni rahisi zaidi ninapoenda kuongea na mashiriki au makampuni kwasababu ninalofanya linathaminiwa lakini pia hata kwa vijana wenzangu sasa hivi itakuwa rahisi kwangu kufanya nao kazi kutokana na kile ninachokifanya kwani nina mipango mikubwa zaidi ya hapo lengo langu ni kafanya process nzima ya kusoma iwe rahisi zaidi na wanafunzi wawe wanapenda zaidi kusoma kwasababu sasa hivi wanafunzi wengi wanachukulia kusoma kama adhabu kuliko kama zawadi..’alisema
Wa pili ni Angel Benedicto ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa ndani (House Girl) alimaliza kidato cha nne akaona aweza kuendelea na masomo, hali ni ngumu kwenye kimaisha akawa ni mfanyakazi wa ndani au msichana wa kazi za ndani (House Girl) lakini leo hii ameweza kutumia nguvu yake ya ushawishi ya kuongea na vijana na kazi yake imetambuliwa na malkia na akapewa tuzo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo July 1, 2015 Angel Benedicto alisema…’Tuzo hii inanisaidia kwamba niweze kuwafikia vijana zaidi ambao ni wafanyakazi wa nyumbani hasa wa kike ambao wamekata tamaa tuweze kuwasaidia kwamba haujazaliwa kuwa mfanyakazi wa nyumbani tu , kuna nafasi nyingi pia kwa hiyo kama ni ujasiriamali jitahidi kama unapata elfu 40 yako tunza…
Unaweza ukabonyeza play kusikiliza walichokizungumza Given na Angel
Tazama video ya sehemu ya tukio…
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.