Yemi Alade ni msanii maarufu kutoka Nigeria ambaye alitamba sana na ngoma yake Johnny. Nimekutana na interview moja aliofanya msanii huyu jijini Lagos, aliulizwa maswali mengi lakini moja kubwa lilikuwa linahusu hali ya wasanii kupeana support kwenye muziki.
Yemi Alade alikuwa na haya ya kusema.
>>> “siwezi kuzungumza kwa niaba ya kila mtu so nitaongea kulingana na mtazamo wangu, kwa mimi binafsi nahisi kwenye industry wanaume wanapeana support zaidi kuliko wanawake, sijui kwa nini ila naona hii ndio hali halisi kwa hapa kwetu.”
>>> “wanaume wanapeana support kirahisi sana… kwa mfano mwanaume kumshirikisha mwanaume mwenzake ni rahisi sana, wanaweza tu wakawa wanapiga stori alafu stori za studio zikazuka mmoja akamuelezea mwenzake shida yake na vitu kama hivyo, basi kupitia kusadiana unakuta wameshirikiana kwenye wimbo”.
>>> “wanawake sasa, kwanza tunazinguana mno na kupeana wakati mgumu… mara utasikia niko studio mummy nitakucheki nikitoka, na hata wakishirikiana wataleta ushindani flani, watafika kwenye show mida tofauti, yote makusudi tuu, kutafuta attention na tunasahau kazi ni yetu sote. Wanaume hawako hivi”. <<< Yemi Alade.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.