Ralph R. Debbas, ni mkurugenzi wa kampuni mpya ya magari W Motors iliyopo Dubai. Na baada ya ujio wao kwenye ulimwengu wa magari, kampuni hii imeanza kutengeneza headlines za kipeke duniani, ikiwa ni kampuni ya kwanza ya kiarabu kutengeneza magari yanayoipiku brand kubwa za magari duniani kama Ferrari, Lambroghini na Buggati.
Toleo la kwanza la gari kutoka kwa W Motors ni supercar Lykan Hypersport, gari lililotokea kuweka headlines kubwa kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram pamoja na internet na headlines zilizopo sasa hivi ni kwamba gari hili laweza kuja kuwa gari la kifarhari kushinda yote duniani.
Nimekusogezea baadhi ya picha za gari hili hapa chini ila na wewe uweze kujionea.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.