Msanii maarufu wa R&B Ciara hivi karibuni alifanya interview kuzungumzia maisha yake ya kuwa mama yakoje na anawezaje kuwa mama na mwanamuziki kwa wakati mmoja… Ciara alikuwa na mengi ya kuongea kuhusu life yake ya sasa hivi.
Kikubwa alichokisema Ciara kwenye interview hiyo ni kwamba ameamua kumuajiri baba yake baada ya kufanya interview nyingi na kukosa dada atakayefaa kushinda na mwanae.
Ciara alitoa na majibu kuhusu malezi yake na mtoto wake.
>>> “Mwanangu yupo na mimi muda wote, na popote nitakapokwenda yeye yupo… Pili mazingira ambayo mimi nipo muda mwingi yamezungukwa na wanawake wengi, nilitaka nihakikishe mwanangu atakuwa kwenye mikono salama“>>> Ciara.
>>> “Nilifanya maamuzi ya kumuajiri baba yangu baada ya kufanya interviews kama 20 na kukosa dada atakayefaa kushinda na mwanangu, sababu nyingine iliyonisukuma kufanya hivi ni mazingira yanayonizunguka kuna wanawake wengi nikaona hii itamuathiri mtoto kisaikolojia“>>> Ciara.
>>> “Kwahiyo nikazungumza na baba yangu, na ilikuwa rahisi kuzungumza nae kuhusu hili kwa sababu anapenda watoto, pili alinilea vizuri na nilihisi uwepo wake utamsaidia sana mwanangu haswa kisaikolojia kwa sababu atakuwa na mtu ambaye anaona yupo kama yeye, baba alikubali“>>> Ciara.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.