Ni utamaduni wa kawaida kabisa na uliozoeleka ikitokea kuna harusi hivi basi kadi za michango zinapitishwa na watu wanatoa chochote ili kusaidia kufanikisha tukio hilo.
Nimefikiwa na hii ya China, unajua kitu kinaitwa Beijing Size Olympic Wedding Expo? umewahi kusikia chochote kuhusu hilo?
Beijing Size Olympic Wedding Expo ni mnada unaofanyika mara tatu kila mwaka ndani ya China… hapo kinaletwa kila kitu kinachohusiana na harusi, iwe ni magauni, suti, pete, mapambo, hadi magari ya maharusi unaweza kuvipata kwenye mnada huo.
Wenyewe wanasema lengo hasa la kufanya mnada huo ni kusaidia kupunguza gharama za matumizi ya pesa zinazotumika kuaanda sherehe hizo.
Lakini kuna baadhi ya Wachina wanaona kuwa mnada huu bado ni kitu cha bei kubwa kwao,wao wameamua kuanzisha style mpya ya kufunga ndoa zinazoitwa Do-It-Yourself Wedding! Aina hizi za harusi hufanyika majumbani na ndugu, jamaa na marafiki.
Harusi za namna hii hazihitaji mialiko kwani mialiko hutolewa kwa njia ya tangazo la bango kwenda kwa ndugu jamaa na marafiki, na MC anaweza kuwa mtu yoyote aliyealikwa. Chakula kinapikwa na wanafamilia na suala la vinywaji linasimamiwa na marafiki.
Nimekusogezea baadhi ya picha za mnada huo pamoja na baadhi ya picha za aina hii ya Do-It-Yourself Wedding.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.