Premier Bet
TMDA Ad

Mix

Badala ya michango ya harusi angalia hiki kinachofanywa na Wachina kwenye ndoa..

on

harusi

Ni utamaduni wa kawaida kabisa na uliozoeleka ikitokea kuna harusi hivi basi kadi za michango zinapitishwa na watu wanatoa chochote ili kusaidia kufanikisha tukio hilo.

Nimefikiwa na hii ya China, unajua kitu kinaitwa Beijing Size Olympic Wedding Expo? umewahi kusikia chochote kuhusu hilo?

chiii

Huu ndio mnada wa Beijing Size Olympic Wedding Expo, mnada wa vitu vya harusi unaofanyika China kila mwaka.

Beijing Size Olympic Wedding Expo ni mnada unaofanyika mara tatu kila mwaka ndani ya China… hapo kinaletwa kila kitu kinachohusiana na harusi, iwe ni magauni, suti, pete, mapambo, hadi magari ya maharusi unaweza kuvipata kwenye mnada huo.

Wenyewe wanasema lengo hasa la kufanya mnada huo ni kusaidia kupunguza gharama za matumizi ya pesa zinazotumika kuaanda sherehe hizo.

00000

Watu wakiwa mnadani wakichagua na kujaribu pete za ndoa zitakazowafaa.

fff

Kwenye mnada kuna baadhi ya magari ya kifahari kabisa ambayo huwekwa kwa ajili ya kusaidia watu kuchagua na kuyakodisha kwa bei poa kabisa.

Lakini kuna baadhi ya Wachina wanaona kuwa mnada huu bado ni kitu cha bei kubwa kwao,wao wameamua kuanzisha style mpya ya kufunga ndoa zinazoitwa Do-It-Yourself Wedding! Aina hizi za harusi hufanyika majumbani na ndugu, jamaa na marafiki.

china

Harusi hii ilifanyika nyumbani kwa hawa wanandoa.

777777

Bwana harusi (wa pili kutoka mwisho) akiwa kwenye pozi ya picha ya pamoja na marafiki zake.

Harusi za namna hii hazihitaji mialiko kwani mialiko hutolewa kwa njia ya tangazo la bango kwenda kwa ndugu jamaa na marafiki, na MC anaweza kuwa mtu yoyote aliyealikwa. Chakula kinapikwa na wanafamilia na suala la vinywaji linasimamiwa na marafiki.

001

Tangazo hili la bango ndio lilitumika kama kadi ya mualiko kwenye harusi hii.

Nimekusogezea baadhi ya picha za mnada huo pamoja na baadhi ya picha za  aina hii ya Do-It-Yourself Wedding.

222222

Hii ndio reception ya harusi hii nyumbani kwa hawa wanandoa kama unavyoona mtu wangu, vitu simple tu maharusi wakiwa kwenye vazi lao la harusi.

003

Ndugu, jamaa na marafiki walioalikwa kwenye harusi hii wako happy kabisa yani.

cnnx

Ni mwendo wa soda na bia za kopo pamoja na juice vyote vikiwa vimeandaliwa na familia na marafiki

4444444

Hapa ni mnadani, nguo za harusi zinachaguliwa.

002

Watu wakiwa mnadani busy na kuchagua pete na vitu vingine vitakavyowafaa.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments