Pata picha unaingia Benki unakutana na kila mtu ndani kavaa kinyago cha kuficha uso mtu wangu?
Jamaa wako serious kabisa China, Kampuni moja iliyopo Handan, Kaskazini mwa Jimbo la Hebei, China wameamua kuweka siku moja rasmi kabisa kwa ajili ya Wafanyakazi kuvaa vinyago usoni ili wapumzike kutabasamu !!
Ishu iko hivi, unajua kuna watu unawakuta wanahudumia sehemu alafu masharti au utaratibu wa kazi wanatakiwa muda wote watoe tabasamu kwa wateja, pata picha sasa kama ni Wafanyakazi wa Hoteli au Benki wanapumzisha saa ngapi nyuso zao kutabasamu??
Hiyo Ofisi ya Wachina wakaona isiwe shida, wafanyakazi wao wanaruhusiwa siku moja kutoa huduma siku nzima wakiwa wamevaa vinyago ili sura zipumzike kuonesha tabasamu !!
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.