Taarifa za usajili ndio kitu ambacho kimekuwa kikitengeneza headlines nyingi kwenye vyanzo vya taarifa za kimichezo hususan mchezo wa soka barani ulaya na mojawapo kati ya taarifa ambazo leo (alhamis) zimeonekana kuwavuta wengi ni hii hapa .
Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wamefikia makubaliano na klabu ya Juventus juu ya usajili wa kiungo hodari raia wa Chile Arturo Vidal ambapo kiungo huyo sasa anatarajiwa kujiunga na wababe hawa siku chache zijazo .
Ripoti nchini Italia zinasema kuwa Bayern imekubali kulipa paundi milioni 40 kwa ajili ya kiungo huyo tegemeo ambaye ataingia Bayern kuziba pengo la kiungo mkongwe Bastian Shcweisteiger ambaye amesajiliwa na Manchester United .
Arturo Vidal aliwahi kucheza nchini Ujerumani kwenye klabu ya Bayer Leverkusen na aliwahi kuingia makubaliano ya kujiunga na Bayern Munich miaka kadhaa iliyopita lakini makubaliano hayo hayakutimia .