Wikiend iliyopita kulikua na story kuwa Amin amezinguana na mchizi wake Msechu na kudai hatamuandikia tena ngoma zake…mwenyewe amesikika kwenye 255 ya Clouds FM na kukana shutuma hizo huku akisisitiza wana uhusiano mzuri tu hadi sasa.
Amesema si kweli hatamwandikia bali kwa sasa hawezi kundika wimbo wowote bila mkataba..
Chege amesema Diamond amemsaidia kumpata Mr. Miyagi toka kundi la Uhuru na kufanya naye kazi…amesema anashukuru kwa msaada na moyo wake bila kuwa na kinyongo…amesema ni mwimbaji wa kipekee hivyo amefurahi kufanya naye kazi…pia amefanya hivyo ili kupata connection za mbali zaidi.
Baada ya Diamond kushinda tuzo ya MTV kisha katupia video ikimuonyesha Jokate akicheza nyimbo ya ‘Mdogomdogo’ ikiwa na maneno ambayo Jokate hakuridhika nayo…baadaye Jokate alimjibu kuhusu video hiyo…baada ya Diamond kutoa Bongo kafunguka na kusema amesikitishwa na post ya Jakote na kusema alimpost kama shabiki.
Amesema huo ni unafki kwani tangu aanze kuwania tuzo za MTV mama, Jokate hajawahi kumsapoti na amepandikizwa chuki na watu anaowajua mwenyewe,
Wasikilize hapa…
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.