Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na kati maarufu kama CECAFA limetangaza mabadiliko ya muda wa kuanza kwa mechi za robo fainali ya michuano hiyo.. CECAFA imetangaza mabadiliko hayo kupitia kwa msemaji wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Baraka Kizuguto.
Mabadiliko yaliotangazwa hapo ni ya mechi za robo fainali, mchezo wa kwanza utapigwa saa 7:45 ambapo itakuwa mechi kati ya APR ya Rwanda dhidi ya Al Khartoum ya Sudan na mchezo wa pili utapigwa saa 9:45 utakutanisha timu ya Gor Mahia ya Kenya dhidi ya Malakia ya Sudan Kusini, michezo hiyo itapigwa July 28.
July 29 itapigwa michezo miwili wa kwanza utakuwa mchezo kati ya KCCA ya Uganda dhidi ya AL Shandy ya Sudan saa 7:45 na mchezo wa pili ni kati Azam FC dhidi ya Yanga saa 9:45 michezo yote itapigwa katika Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam na hakutakuwa na dakika 30 za nyongeza kama timu zitatoka suluhu bali zitapigiana mikwaju ya penati.
Sambamba na mabadiliko hayo CECAFA pia imewaandikia barua ya kuwapa onyo klabu ya Gor Mahia ya Kenya na kocha wao Frank Nutall kwa utovu wa nidhamu kwa kutumia mlango ambao hawakupaswa kutumia wakati wa kuingia na kutoka vyumbani.
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.