Baada ya kucheza kwa muda mrefu katika klabu ya Dar Es Salaam Young African Jerson Tegete ameachana na timu ya Yanga na sasa ni mchezaji huru, team ya millardayo.com ilimtafuta iliiweze kufahamu Tegete atacheza wapi msimu ujao na nini kilikuwa kinamnyima namba katika kikosi cha kwanza Yanga.
Tegete ameichezea Yanga kwa miaka saba lakini yeye pamoja na Mrisho Ngassa miongoni mwa wachezaji waliopata bahati ya kufanya vizuri katika timu ya Taifa 2006 ikiwa chini ya kocha wa kibrazil Marcio Maximo, Tegete pekee ndiye aliyeonekana kutofanya vizuri na amekiri hali hiyo imetokea kwa sababu amekuwa akisumbuliwa na goti kwa miaka minne.
Hata hivyo Tegete amekiri kuwa na mahusiano mazuri na Mrisho Ngassa kiasi cha kusema Ngassa ameshawahi kujaribu kumtafutia Connection licha ya Ngassa kuwa anatafutiwa pia nafasi za kucheza na kufanya majaribio katika nchi mbalimbali.
“Kwanza mimi nasema kilichonifanya nikose namba Yanga ni majeruhi nimekuwa majeruhi kwa muda mrefu lakini sasa nimepona nitapata nafasi nitaonyesha uwezo sehemu nyingine, Ngassa ni zaidi ya rafiki sababu toka wadogo tumekuwa pamoja kwa hiyo lazima tushirikiane kwa kila kitu sio soka tu hata nje ya soka”>>>Tegete
Jerson Tegete ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa soka John Tegete ambae kwa sasa ni kocha wa timu ya Toto African ya Mwanza ila Tegete licha ya kuwa hana timu hadi sasa Tegete amekiri kutokuwa na lengo la kucheza timu inayofundishwa na baba yake hivyo ana mipango mingine katika soka.
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.