Mwanzoni mwa mwezi July kulikuwa na habari mbalimbali zilizoweka headlines katika mitandao ya kijamii kuhusu mchezaji wa Yanga Simon Msuva na baba yake Mzee Msuva, kila mtu alikuwa anazungumza kuhusiana na Simon Msuva.
August 3 Simon Msuva aliongea na millardayo.com na kuweka wazi kuhusiana na taarifa za yeye kupuuza ushauri wa baba yake, awali kulikuwa na uvumi kuwa baba yake Simon Msuva alimshauri aondoke Yanga na kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine hususani klabu ya Simba ambayo baba yake ndio klabu anayoipenda.
Msuva amezungumzia hizo taarifa za baba yake kutaka aondoke Yanga >>> “kiukweli Mzee anamapungufu yake siwezi kumuongelea sana sababu yeye sio mtu anayeniongelea mimi, mtu anayeniongelea mimi ni Management yangu ambayo inaweza ikaongea kila kitu kuhusu mimi”
“kwa hiyo mzee anaweza ongea chochote kama mzazi, mzee kama mzee anaweza akawa kaongea ila watu wakamuelewa vingine. Mzee hawezi kuongea sitaki mwanangu acheze Yanga aende nje au acheze Simba hicho kitu nakataa inawezekana waandishi labda wakawa wamemuuliza hivyo inategemea si unajua waandishi wanavyouliza ” >>> Simon Msuva
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos