Hekaheka ya leo ni mwendelezo wa ile ya jana iliyotokea maeneo ya Kigogo, Dar es salaam ambapo jamaa mmoja alifumaniwa baada ya kuingia chumbani kwa mpangaji mwenzake ambaye ni mke wa mtu baada ya mke wake kwenda kwao kujifungua..lakinialijitetea alikwenda kuchukua pasi
Leo mke wa mume aliyefumaniwa amesema hata yeye aliwahi kuhisi hicho kitu tangu muda mrefu..anasema huyo dada alianza kumtolea mafumbo na ikafika kipindi mume wake anatoroka usiku bila kuaga na kushindwa kujua amekwenda wapi na akiwa anarudi akiulizwa anasema ametoka chooni.
Anasema dada huyo alikua rafiki yake mkubwa lakini ilifika kipindi rafiki yake huyo akitoka haagi na akiwa ana rudi, akikaa kidogo na mume wake anaingia na kuhisi walikua pamoja.
Wasikilize hapa akizungumza kwenye HekaHeka…
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos