Nahodha wa Dar Es Salaam Young African pamoja na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Nadir Haroub Cannavaro amezungumzia kuhusiana na zile taarifa za yeye kuhitajika na klabu ya Al Ahly ya Misri ambazo ziliishia kimya kimya. Cannavaro alihusishwa kujiunga na klabu ya Al Ahly baada ya kuonekana uwezo wake kwenye mechi ya Yanga dhidi ya Al Ahly.
Cannavaro uwezo wake ulionekana katika mchezo wa pili wa marudiano uliochezwa mwanzoni mwa mwaka 2014 Misri ambapo Yanga ilifungwa goli 1-0 nakulazimika kwenda katika hatua ya mikwaju ya penati baada ya ule mchezo wa awali uliopigwa Dar Es Salaam kumalizika kwa Yanga kushinda goli 1-0.
Cannavaro kama mmoja wa watu walioonyesha uwezo mzuri katika dakika zote 90 na hata katika hatua ya mikwaju ya penati uwezo wake uliwavutia viongozi wa Al Ahly ya Misri kiasi kwamba walienda hadi hotel waliofikia Yanga na kuongea na kiongozi wa Yanga.
“Ilikuwa ni kweli ila uongozi wetu sisi na Al Ahly kidogo ulikuwa sio mzuri kutokana na yule kocha alitufuata hotelini na aliongea na Vice president wetu na baada ya hapo mazungumzo yalikuwa yameenda vizuri ila yule kocha alifukuzwa Al Ahly ndio maana ikawa kidogo imekatika ila tu maendeleo yalikuwa mazuri sana kutokana kwamba Yanga walikuwa wanahitaji milioni 200 kama sikosei”>>> Cannavaro
Nikukumbushe tu mtu wangu ilivyokuwa katika mchezo na penati ya Cannavaro
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos