Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa leo ametangaza kikosi cha wachezaji 29 watakaongia kambini Jumapili katika hoteli ya Tansoma kwa ajili ya kambi ya wiki moja ya mazoezi.
Katika kikosi hicho alichokitangaza cha wachezaji 29, Mkwasa amewajumuisha wachezaji watano wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, ambao baadaye watajumuika kwa kambi ya kujiandaa kucheza na Nigeria mwezi Septemba 2015.
Taifa Stars inatarajiwa kuweka kambi ya siku kumi Jijini Istanbul, Uturuki ambapo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za Taifa za Libya na Kuwait kabla ya kurejea nchini kuwavaa Nigeria.
Wachezaji watakaongia kambini Jumapili ni makipa, Ally Mustafa ‘Barthez’ wa Yanga SC na Aishi Manula wa Azam FC.
Mabeki ni Shomari Kapombe (Azam FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Juma Abdul, Mwinyi Haji (Yanga SC), Hassan Isihaka (Simba SC), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani (Yanga SC).
Viungo ni Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Salum Telela (Yanga SC), Abdi Banda na Said Ndemla wote wa Simba SC… Mawinga ni Orgenes Mollel (Aspire – Senegal), Abdrahman Mbambi (Mafunzo), Deus Kaseke, Simon Msuva (Yanga SC), Ramdhani Singano na Farid Mussa (Azam FC), wakati washambuliaji ni John Bocco, Ame Ally (Azam FC) na Rashid Mandawa (Mwadui FC).
Wachezaji wanaocheza nje waliojumuishwa katika kikosi hicho ambacho Agosti 23 kitaelekea kambini nchini Uturuki kwa kambi ya siku kumi ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – DRC), Mrisho Ngassa (Free State – Afrika Kusini) na Hassan Sembi (Santos FC – Afrika Kusini) na Adi Yussuf (Mansfield Town – England).
Msikilize Mkwasa hapa akitaja majiya ya wachezaji 29
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos