HekaHeka ya leo inamuhusu mwanamuziki Badi Bakule ambaye amezungumzia kuhusu changamoto za kuigiza akiwa ndani ya jeneza, anasema jambo hilo lilikuwa zito na kwa sasa hawezi kurudia kitu kama hicho.
Anasema pia maamuzi yake hayo alishindwa kuwashirikisha familia yake akiwemo mke wake na walikuja kuona kwenye TV na magazeti..alifanya hivyo kutokana na kazi yake ambayo lazima aweze kuigiza kitu chochote kwa kuwa ni sehemu ya kazi yake.
Bakule hakuishia hapo amesema baada ya kumaliza kuigiza walirudisha sanduku kwa fundi Seremala licha ya kulinunua kwa pesa nyingi kwa kuwa hawakua na kazi nalo tena na nguo alizokua amevaa wakati anaigiza alizichana na kutupa.
Msikilize hapa akizungumza na HekaHeka…
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos