Nimekutana na interview moja aliyofanya kaka yake Tupac Shakur, Mapreme Shakur siku chache zilizopita na moja ya vitu alivyoulizwa kwenye interview hiyo ni kama ni kweli Janet Jackson alikataa kufanya scene ndogo ya movie na 2Pac mwaka 1992 mpaka apime UKIMWI...
Kwenye interview Mopreme Shakur aliulizwa >>> “Nilisikia stori moja kuhusu movie ya 2Pac ya Poetic Justice kuwa Janet Jackson alikataa kufanya scene ya mapenzi na 2Pac mpaka apime UKIMWI kitu kama hicho?<<<
Mopreme alijibu hivi.. >>>“haha haikuwa scene ya mapenzi ilikuwa scene ndogo ya Janet kumpatia kiss 2Pac, na siku chache kabla ya siku ile Janet alikuwa ametoka kushoot movie nyingine alafu akaumwa mafua…sio kwamba aliyekuwa nae alimuambukiza lakini ilitokea tu alipata mafua…sasa akamwambia 2Pac ooh unajua itabidi ukapime UKIMWI kwanza ndio tukiss sio kwa ubaya lakini…2Pac hakuelewa kabisa..hakuelewa!”<<< Mopreme Shakur.
>>>“alisema kama nitakuwa nae kimapenzi baada ya hapa basi sawa nitapima UKIMWI lakini kwa kitu kidogo kama hiki nikapime UKIMWI kwanini!? 2Pac hakupenda ile kauli kabisa…ilikuwa tabu ila badaae waliyamaliza..so yeah ilishawahi kutokea.”<<< Mopreme Shakur.
Hapa chini nimekusogezea sauti ya Mopreme Shakur akielezea jinsi ilivyokuwa kipindi hicho kati ya Janet Jackson na kaka yake.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos