Vodacom wamekuwa wakidhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa zaidi ya miaka nane, ninayo good news tena kutoka kwao leo !!
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF August 12 2015 limeingia mkataba wa udhamini na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom wa kuendelea kuidhamini Ligi Kuu Tanzania ambapo Mkataba huu mpya ni wa miaka mitatu
Mkataba huo ulisainiwa ambapo upande wa TFF uliwakilishwa na Rais wao, Jamal Malinzi na Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Borniface Wambura huku upande wa Vodacom ukiwakilishwa na meneja masoko wa kampuni hiyo, Kelvin Twissa.
Mkataba wa sasa umeberoshwa kwa kiwango cha fedha kwani uliomalizika ulikuwa na thamani ya bilioni 1.6 huku huu wa sasa umeongezeka kwa asilimia 40 zaidi ya ule wa awali nakufanya thamani yake kuwa bilioni 2.3.
“TFF tunayo furaha kubwa kukaa na ndugu zetu wa Vodacom katika kuhitimisha kile tulichokuwa tunakifanya kwa muda wa mwaka mzima, Mungu ametusaidia leo hii tunasaini mkataba mwingine wa miaka mitatu utakaotupeleka kwa kipindi cha msimu huu na 2016-2017 na 2017- 2018 “>>>Jamal Malinzi.
“Ligi zipo zaidi ya nane ukitoa Premier League.. mwenye interest ya kuingia kwenye mpira aingie lakini kuniambia leo hii mimi niruhusu mwingine aingie hapana tunadhamini hii kitu ili kukuza biashara yetu na kusaidia soka“>>> Kelvin Twissa
Nimekusogezea sauti ya Rais wa TFF Jamal Malinzi na Meneja masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos