Leo tunaendelea na ile HekaHeka ya jana ambayo baba mmoja alikua akilalamika kuhusu mke wake kuwa na uhusiano na mwanaume mwingine ambaye ni wa asili ya Kihindi na kuitelekeza familia yake.
Baada ya jana kusikiliza malalamiko kutoka kwa mwanaume huyo, leo timu ya HekaHeka ilimtafuta mke wake na kuzungumza ambapo amesema yeye ameamua kuondoka nyumbani kwake baada ya kuwepo malumbano ya muda mrefu na mume wake huyo.
Anasema si kweli kuwa ana uhusiano na mwanaume mwingine bali yeye ameamua kuondoka na kwenda kupanga sehemu nyingine na amekua akiwasiliana na watoto wake ingawa amekiri kuwa hawezi kurudi kukaa nyumbani kwake.
Mwanaume anayedaiwa kumchukua mke wa mtu amesema si kweli kuwa ana uhusiano na mwanamke huyo na amekua akishangangazwa na uvumi huo.
Wasikilize hapa…
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos