Producer wa Birdman, DVLP anamshitaki rapper huyo dhidi ya deni la dola 200,000 (sawa na Tzs. Million 400) kwa kazi za production ambazo boss huyo wa Cash Money Records hakumlipa.
Producer DVLP ndiye aliyesimamia wimbo wa “develop” lakini Birdman hakuwahi kumlipa kwa kazi hiyo aliyoifanya na Lil Wayne pamoja na wasanii wengine… hata hivyo producer huyo anadai walishawahi kuzungumza na Birdman kwa message za kuchat kwenye simu lakini hakuwahi kutoa ahadi ya lini atamlipa pesa hizo.
Kazi ya kwanza ya DVLP ilikuwa na Lil Wayne mwaka 2005 kwenye ngoma ya “Fireman” ya rapper huyo na toka kipindi hiko amekuwa akifanya kazi mara kwa mara na star huyo wa Cash Money Records.
Licha ya kufanya kazi na Lil Wayne, DVLP ameshawahi pia kufanya kazi na rapper Rick Ross kutoka Maybach Music Group na Pitbull na alishawahi pia kutengeneza beat ya ngoma “Rap God” kwa ajili ya Eminem.
Producer DVLP ameamua apeleke mashitaka yake Mahakamani kwani ameona kama dalili za yeye kulipwa pesa zake ni ndogo ukizingatia mvutano uliopo sasa kati ya Birdman na Lil Wayne upo mbali na mwisho.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos