August 19 Afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura ametangaza ratiba rasmi ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara ambapo Ligi Kuu itaanza Septemba 12 2015 ambapo itakuwa ni wiki moja baada ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kucheza na timu ya taifa ya Nigeria mchezo wa kufuzu AFCON 2017.
Wambura amethibitisha kupangwa kwa ratiba ya Ligi hiyo kwa kuzingatia mazingira ya timu zinakotoka na sehemu zinakoenda ili kuvisaidia vilabu kupunguza gharama za nauli, ratiba pia imepangwa kwa kuzingatia timu zitakazoshiriki klabu Bingwa barani Afrika na kombe la shirikisho.
Hata hivyo Wambura alitangaza pia kuanza kwa kombe la FA ambapo litashirikisha timu 64, timu 16 za Ligi Kuu, timu 24 za Ligi daraja la kwanza na timu 24 za Ligi daraja la pili kwani ujio wa Kombe la FA unakuja sambamba na neema ya kupatikana kwa mdhamini wa Kombe la FA.
Ratiba ya Kombe la FA itatoka baada ya kutoka kwa ratiba za Ligi daraja la kwanza na Ligi daraja la pili kwani timu shiriki zinategemea viwanja ambavyo pia vitatumika katika michezo ya Ligi Kuu.
“Msimu wa Ligi umeshafunguliwa kwa maana ya usajili ila kwa mashindano tutaanza kucheza Septemba 12 na tutamaliza mzunguko wa kwanza Novemba 7 baada ya hapo tutaingia katika usajili wa dirisha dogo kupisha michuano ya Challenge Cup na tutaendelea December 19 na tutaenda kumaliza Ligi Mei 7 2016″>>>Wambura
Hii ndio ratiba yote ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2015/16.
Hii ni sauti ya Wambura wakati akitoa Ratiba hiyo na mengine aliyoyazungumza Dar es Salaam August 19 2015.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos