Stori za Siasa na uzito wake, zinatufikia mpya kila siku na kila mpya inayonifikia na mimi nakusogezea… hii imenifikia dakika chache zilizopita kutoka Bahari Beach Dar es Salaam, Ukumbi uleule ambao July 28 2015 Mbunge wa Monduli anayemaliza muda wake na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa alitangaza kujiunga CHADEMA, leo Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Tluway Sumaye naye ametangaza kujiunga na Umoja wa Vyama vya UKAWA.
Frederick Tluway Sumaye ametumikia miaka kumi kwenye nafasi ya Uwaziri Mkuu wakati Mzee Benjamin William Mkapa akiwa Rais wa Tanzania kuanzia mwaka 1995 mpaka 2005… kwenye nilichomnukuu wakati akitangaza uamuzi huo kuna hizi sentensi pia.
‘Niligombea Urais CCM kutaka kurekebisha Utawala na kujenga Chama mbadala wa CCM’- #FrederickSUMAYE #UKAWA #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) August 22, 2015
‘Sitoki CCM kwa ajili ya kukidhoofisha Chama, Watz wanajua umuhimu wangu lakini CCM hawajui’- #FrederickSUMAYE #UKAWA #MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) August 22, 2015
‘Natoka CCM ili kuimarisha Upinzani, sijiungi kwa maslahi binafsi, sijadai fedha wala cheo’- #FrederickSUMAYE #UKAWA #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) August 22, 2015
‘Kwa mafuriko tunayoyashuhudia leo, kuna dalili UKAWA ikashinda sana’-#FrederickSUMAYE #UKAWA #MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) August 22, 2015
‘Natamani watu wenye nia njema walioko CCM waje wasaidie UKAWA.Kuzuia mageuzi ni kazi ngumu sana’-#FrederickSUMAYE #UKAWA #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) August 22, 2015
‘Natangaza rasmi kuhamia UKAWA, kuhusu Chama gani nitawaambia baadaye. Asanteni sana’- #FrederickSUMAYE #UKAWA #MillardAyoUPDATES — millard ayo (@millardayo) August 22, 2015
Sauti yake nimeirekodi na kukuwekea hapa pia mtu wangu.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos