Mpambano uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka Tanzania kati ya klabu ya Yanga dhidi ya Azam FC,huu ni mchezo wa ngao ya hisani umechezwa siku ya Jumamosi ya August 22. Mchezo huu ambao kila timu imepania kulinda heshima kwani ni mechi inayowakutanisha mabingwa wa Ligi Kuu Yanga dhidi ya Azam FC ambayo ni mshindi wa pili wa Ligi Kuu Tanzania bara.
Mchezo ambao ulikuwa wa kuvutia na kushambuliana kwa zamu, kipindi cha kwanza kilimalizika kila timu ikienda mapumzikoni bila kuona lango la mwenzake. Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kushambuliana kwa zamu. Mchezo uliamuliwa kwa mikwaju ya penati na Yanga kuibuka na ushindi wa penati 8-7.
Penati za Yanga zilipigwa na Mbuyu Twite, Amissi Tambwe, Geofrey Mwashiuya, Andrey Coutinho, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Kelvin Yondani huku Nadir Haroub akikosa penati na penati za upande wa Azam FC zilipigwa na Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Himid Mao, John Bocco, Kipre Tchetche, Jean Mugiraneza na Pascal Wawa na Ame Ally penati zao zilidakwa na Ally Mustapha
Hizi ni picha za mchezo mtu wangu
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos