Imepita miaka 4 toka msanii wa muziki wa Pop kutoka Uingereza Adele aachie album yoyote. Baada ya album yake ya mwisho ’21’ ya mwaka 2011 Adele alitangaza kuwa hatotoa album yoyote mpaka mwaka 2015.
2015 ndio hii hapa na sasa tunaelekea mwishoni mwa mwaka na bado hatujasikia wala kuona kitu chochote kutoka kwa Staa huyu wa ‘Set Fire to The Rain’.
Good news kwako mtu wangu, kama wewe ni miongoni mwa mashabiki wazuri wa Adele basi taarifa hii ikufikie kokote kule uliko…mtandao wa Billboard wa Marekani umetangaza kuwa Adele atarudi kwenye headlines za burudani mwezi November na album mpya iliyopewa jina ’25’.
Tarehe ya uzinduzi wa Album hiyo haijatajwa bado ila taarifa ya uhakika ni kwamba album hiyo itazinduliwa kupita lebo yake XL Recordings iliyopo Uingereza.
Hii itakuwa album ya 3 ya Adele toka aanze safari yake ya muziki, Album yake ya kwanza ’19’ ilitoka mwaka 2008 na iliuza zaidi ya copy million 7 dunia nzima, Album yake ya 2 ’21’ iliyobeba nyimbo kama ‘Someone Like You’ ‘Rumor Has it’ na ‘Set Fire to The Rain’ ya mwaka 2011 iliuza copy million 30 dunia nzima.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos