Hekaheka ya leo inatokea hapa hapa Dar.. inamuhusu mke mkubwa na mke mdogo kugombea nyumba ya urithi waliyoachiwa na marehemu mume wao,Nyumba alikuwa akiishi mke mdogo.
Wakati kesi tayari ipo mahakamani na hukumu inakaribiwa kusomwa, Mke mkubwa na ndugu zake wakaambiwa na mtu kwamba mke mdogo kafukia mbuzi wa kishirikina ili kesi isiwepo.
Waakamua kwenda eneo la tukio na kwenda kufukua uyo mbuzi aliyefukia, waliwatafuta vijana kwa ajili ya kufukua wakiwa wamebeba chumvi na haja ndogo kama walivyoambiwa ili wasidhurike.
Baada ya vijana kufukua wakashangaa kukutwa ni mbwa aliyekufa, ikabidi wamrudishe kumzika na kuamua kuondoka zao.
Isikilize hapa..
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos