Kila siku team ya Hekaheka kutoka Clouds FM imekua ikituletea matukio mbalimbali yanayotokea ndani ya familia zetu.
Hekaheka ya leo inatokea Kahama ambapo mtoto wa miezi mitano aling’atwa na punda na kisha kukimbia naye umbali wa mita kama 300.
Shuhuda wa tukio hilo amesema mtoto huyo alikua amelala pembeni ya kibanda cha mama yake ambaye alikua anapika mara ghafla punda mmoja akaja kisha akamng’ata, akaanza kukimbia naye.
Mama wa mtoto amesema alikuwa amemkalisha chini huku yeye anapika, lakini akashangaa punda amemchukua mtoto wake na kuanza kukimbia naye.
Anasema baada ya mwendo mrefu yule punda alikutana na mtu mwenye fimbo ndipo akamuachia yule mtoto lakini akiwa tayari na majeraha mbalimbali na mpaka sasa amelazwa katika hospitali ya Kahama.
Daktari wa mifugo amesema punda pia anaweza kupata kichaa cha mbwa hivyo ni vyema wananchi wakajua hilo, pia anaweza kufanya hivyo akiwa katika wakati wa kutaka kujamiana.
Baada ya tukio lile wananchi wenye hasira waliwakamata wale punda wote wawili na kuwachoma moto.
Isikilze Stori nzima hapa kwenye Hekaheka…
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos