Rapper wa Marekani Kanye West ambaye ni baba wa mtoto wa kike North West, mtoto aliyempata kwa staa wa kipindi cha Keeping Up With the Kardashians Kim Kardashian, ametangaza kwa kushtukiza kufanya New York Fashion Week Show kitu kilichopelekea wabunifu wengine wa mavazi kubadili tarehe ya Fashion Show zao.
Anne Bowen ambaye ni mbunifu wa mavazi amebadili tarehe ya onyesho la mavazi yake licha ya kuwa alikuwa amefanya uwekezaji mkubwa katika kipindi cha mwaka mzima kwa ajili ya Fashion Show yake. Maamuzi hayo ya Anne Bowen yamekuja baada ya Kanye West kutangaza kwa kushtukiza kufanya Fashion Show.
Kanye West ambaye ni mkali wa ngoma kama Bound 2 na Mercy aliyowashirikisha Big Sean, Pusha T na 2 Chainz ataonyesha toleo la pili la mavazi yake ya Kanye West X Adidas Originals Collection, kutokana na ukubwa wa jina la Kanye West. limemfanya Anne Bowen kubadili tarehe ya Fashion Show yao kwani huenda ikakosa watu. Hii ni stori kutoka dailymail.com.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos