Nimekutana na stori kutoka Thailand inayomhuusu mwanamke mmoja kutoka China kukamatwa na almasi tumboni mwake…
Jiang Xulian ni raia wa China ambaye aljikuta matatani na polisi baada ya yeye na mchumba wake wa Kichina kukiri kuiba jiwe la almasi lenye thamani zaidi ya milion 560 za Kitanzania siku ya Ijumaa baada ya jiwe hilo kuonekana kwenye X-ray scan ya mwanamke huyo.
Jiang na mchumba wake walizuiliwa na polisi kwenye uwanja wa ndege wa Bangkok Suvarnabhumi International Airport walipokuwa wanajaribu kutoroka nchi hiyo… taarifa za almasi hiyo ziliwafikia polisi baada ya mkaguzi wa duka liitwalo ’56th Bangkok Gems & Jewelry Fair’ kutoa ripoti ya kuibiwa kwa jiwe hilo kwenye duka hilo.
>>> “Alipewa dawa za kumsaidia kupata choo lakini siku tatu badaae hakuna kilichotokea, na pale polisi walipojaribu kumpatia chakula aligoma kabisa kula bali alisisitiza apewe maji tu!”<<< walisema Polisi kituoni hapo.
Baada ya njia zote za Polisi kugoma, kituo cha polisi kilichokuwa kinamshikilia dada huyo kiliamua kufanya utaratibu wa kupata kibali cha hospitali kitakachowaruhusu madaktari kumfanyia operation mwanamke huyo ili kuitoa almasi hiyo tumboni mwake… madaktari walifanikiwa, na Jiang anashitakiwa kwa kosa la wizi na pengine atakuwa matatani kufungwa kwa miaka 3 na faini juu!
Issue kama hii unaambiwa ishawahi kutokea mwaka 2012 huko South Africa pia baada ya polisi kumkamata mwanaume aliyekuwa anajaribu kutoroka nchini humo na almasi zaidi ya 220 tumboni mwake! Nae kama Jiang alikamatwa uwanja wa ndege baada ya X-ray scan kunasa almasi hizo tumboni mwake!
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata piausisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos