Ikiwa ni wiki moja imepita toka beki wa klabu ya Manchester United, Luke Shaw avunjike mguu wake wa kulia, baada ya kufanyiwa tackling na beki wa klabu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi Hector Moreno, tukio lililopelekea kutolewa uwanjani katika dakika 15 za mwanzo.
Hector Moreno ameingia tena katika headlines ya kucheza faulo mbaya, ambayo ingeweza kumvunja Oussama Tannane wa klabu ya Heracles. Moreno ambaye alimfanyia tackling Luke Shaw na kumvunja mguu wiki iliyopita katika mchezo wa Ligi ya mabingwa Ulaya amefanya faulo ya hatari kwa Oussama Tannane.
Beki huyo wa PSV amecheza faulo hiyo dakika ya 72 ya mchezo, baada ya kushindwa kuumiliki mpira mrefu uliyopigwa kutokea upande wa Heracles kuelekea langoni kwao hivyo Moreno na Oussama Tannane wote walikuwa na asilimia 50 kwa 50 ya uwezekano wa kila mmoja wao kuupata mpira ila Moreno akamkang’anyaga juu ya ugoko Oussama Tannane.
Hii ni video ya faulo aliyomfanyia Oussama Tannane
https://youtu.be/31m4V_q2460
Hii ni video ya faulo aliyomfanyia Luke Shaw usiku wa Sept 15 2015.
https://youtu.be/TJ39f4xbguM
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE