Bado Ligi Kuu soka Tanzania bara inaendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti tofauti, September 30 Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania bara Dar Es Salaam Young African wamesafiri kuifuata Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Hii ni moja kati ya michezo ya kuvutia kwa wapenzi na mashabiki wa soka Tanzania, kwani timu itakayoibuka mshindi wa mechi hii, itapata nafasi ya kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2015/2016, Mtibwa Sugar ambayo ni timu mwenyeji wa mchezo huu imeshinda mechi zake nne za mwanzo kama ilivyo kwa Yanga.
Mchezo ambao ulikuwa wa kukamiana hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika kila timu haikubahatika kuona nyavu za mwenzake, kipindi cha pili Yanga walionekana kubadilika na kuja na mbinu mbadala, Malimi Busungu akapachika goli la kwanza dakika ya 53 ya mchezo, Donald Ngoma ambaye awali alionekana kudhibitiwa na mabeki wa Mtibwa Sugar, alibahatika kuitumia nafasi aliyoipata dakika ya 89 ya mchezo na kuufanya mchezo kumalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa September 30
Simba 1-0 Stand United
Azam FC 2-0 Coastal Union
Prisons 0-0 Mwadui FC
Maji maji 1-1 Ndanda FC
African Sports 0-1 Mgambo Shooting
Kagera Sugar 0-0 JKT Ruvu
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE