July 06 2015 ilisambazwa Taarifa kwenye Vyombo vya Habari kuhusu Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam kutoa hukumu ya kifungo cha miaka mitatu jela kila mmoja kwa Mawaziri wa zamani, Basil Pesambili Mramba, na Daniel Yona baada ya kukutwa na hatia ya Kesi ya kuisababishia hasara Serikali pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.
Mbali na hukumu ya kifungo cha miaka mitatu jela, Mramba na Yona walitakiwa pia kulipa faini ya Milioni tano kila mmoja.
Ninayo Ripoti nyingine kutoka Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam… Rufaa ya Kesi hiyo imefikishwa kwenye meza ya Mahakama ya Rufaa na Mahakama hiyo imeikataa Rufaa hiyo.
Kingine kilichoamriwa ni kwamba watuhumiwa wote wawili wamepunguziwa adhabu ya kifungo, kwa sasa watatumikia miaka miwili jela na adhabu ya faini imeondolewa.
Mahakama imetupa rufaa ya mawaziri wa zamani B.Mramba na D.Yona, yawapunguzia adhabu toka miaka mitatu hadi miwili jela. #MillardAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) October 2, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE