Michezo

Mambo ni moto Chelsea, hiki ndio kinachoendelea kwa Mourinho na wachezaji wake..

on

Baada ya kupoteza mchezo mwingine kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa ukiwa mchezo wa tano kupoteza tangu msimu huu uanze, hali imezidi kuwa mbaya ndani ya klabu ya Chelsea kufuatia mkutano ambao kocha Jose Mourinho aliufanya na wachezaji wake.

Katika mkutano huo inasemekana Mourinho aliwashutumu wachezaji wake akiwataja baadhi kwa majina kwa kile ambacho alikiita kuonyesha kiwango duni ambacho hakiendani na hadhi ya klabu yao.

Mourinho amekuwa mbogo msimu huu huku akiwalaumu wachezaji wake kinyume na ambavyo alikuwa akifanya msimu uliopita wakati klabu hiyo iliposhinda ubingwa wa Ligi Kuu ya England ambapo kocha huyo alionekana kuwa mpole na muelewa.

Uhusiano kati ya Mourinho na wachezaji wake umeingia dosari baada ya matokeo mabaya kwenye michezo ya hivi karibuni .

Mourinho na wachezaji wake.

Katika mkutano uliofanyika kwenye makao makuu ya klabu siku ya jumatano baada ya timu kurudi toka Ureno ambako walifungwa na Fc Porto, Mourinho aliwashutumu vikali wachezaji wake kwa kiwango kibovu na alifikia hatua ya kutishia kuwapanga wachezaji wa kikosi cha pili.

Hali hii imetafsiriwa na wengi kuwa ni shinikizo kubwa ambalo Mourinho anakumbana nalo msimu huu kutokana na Chelsea kushindwa kufanya vizuri kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Nahodha John Terry amejikuta akikalia benchi baaada ya kiwango chake kushuka.

Nahodha John Terry amejikuta akikalia benchi baaada ya kiwango chake kushuka.

Mourinho aliwashutumu wachezaji kama Caesar Azipilicueta, Branislav Ivanovic na Nemanja Matic ambapo alimwambia wazi Matic kuwa amekuwa kwenye kiwango kibovu na anahitaji kufanya mazoezi ya ziada.

Beki Caesar Azpilicueta naye aliambiwa na Mourinho kuwa ana bahati kubwa kwa vile Chelsea haina beki wa kushoto asilia na kama ingekuwa hivyo asingepangwa kwenye kikosi cha kwanza.

Hadi sasa Chelsea imejikuta kwenye wakati mgumu baada ya mfululizo wa matokeo mabaya huku Mourinho akizidi kuwa na uhusiano mbovu na baadhi ya wachezaji wake akiwemo nahodha John Terry ambaye amekuwa akiwekwa benchi.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments