Licha ya Marekani kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa kuwa na Sheria kali zinazodhibiti kudownload nyimbo kinyume na utaratibu uliowekwa, sources nyingi zinazotoa huduma ya kustream na kudownload muziki kama Tidal, Apple Music na Spotify za Marekani bado zinashindwa kudhibiti kwa asilimia mia moja vitendo vya watu kudownload nyimbo za wasanii kinyume na utaratibu na Sheria zilizowekwa! Tatizo ambalo hata kwa hapa kwetu Tanzania lipo sana.
Kwa mujibu wa utafiti mpya uliyofanyika na SeatSmart, soko la kudowload muziki kinyume cha Sheria Marekani halionyeshi dalili la kufa wala kupotea hivi karibuni… utafiti huo umeonesha kuwa muziki wa HipHop ndio unaoongoza kwa kuwa na downloads nyingi sana ambazo zipo kinyume na utaratibu wa kisheria!
Wasanii kama Drake na Future kwa mwaka huu tu wametajwa kuwa wasanii wa HipHop ambao ngoma zao ndio zinazoongoza kwa kuwa na downloads nyingi ambazo hazifuati utaratibu wala Sheria za jinsi ya kudownload nyimbo hizo… kwa mfano Album ya Future ‘DS2’ iliotoka miezi michache iliyopita mwaka huu imeonekana kuwa na downloads nyingi ambazo sio halali kwa siku moja tu ikifuatiwa na ‘IYRTITL’ ya kwake Drake!
Muziki aina ya Pop, Rock, Country, na R&B nazo pia zimetajwa kuwa na idadi nyingi za downloads zilizopo kinyume na Sheria licha ya mipango mingi kuwekwa kudhibiti vitendo hivyo!
Nimefanikiwa pia kuzinasa baadhi ya picha za utafiti wa SeatSmart, zinazoonesha kwa kiasi gani download hizo zinafanyika na kuzisogeza kwako hapa chini…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM,TWITTER,FB, YOUTUBE