Baada ya jana yule msanii wa Rwanda Man Martin kulalamikia kutopewa ushirikiano na Director Nisher baada ya kutua nchini kwa ajili ya kufanya video yake leo inaendelea.
Soudy Brown baada ya kumkosa Nisher mwenyewe, kazungumza na meneja wa kampuni yake aitwaye Helen ambaye amesema si kweli walikataa kumsainisha bila mkataba.
Helen amesema aliwaomba kufanya kazi toka mwezi wa nne na wakaingia mkataba na akalipa ela ya booking dola 1000 lakini hakutokea na juzi alirudi na kutaka asainishwe mkataba mwingine kinyume na makubaliano yao.
Amesema kwa sasa hawataweza kufanya naye tena kazi kwa sababu kwanza amezungumza vitu vya uongo na pia pesa aliyotoa kiasi cha dola 1000 ilikua ni ya booking na si advance kama alivyosema, hataweza kurudishiwa hizo pesa.
Tunaomba radhi kutokana na tatizo la sauti…
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE