Mabingwa wa ligi kuu England Chelsea imepata matokeo mabaya mfululizo na kusababisha kuwa na sintofahamu juu ya kibarua cha kocha wao Jose Mourinho.
Pamoja na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich kukanusha kumtimua kocha huyo lakini ukweli ni kwamba endapo watadhubutu kufanya hivyo itawalazimu kumlipa Kocha huyo kwa kumlipa kiasi cha Euro milioni 30.
Mourinho aliongezewa mkataba mwingine wa mwaka mmoja usiopungua Euro milioni 8.5 na kumfanya kuendelea kubaki ndani ya klabu hiyo hadi mwaka 2019.
Kutokana na matokeo mabaya wanayoyapata kwa sasa mabingwa hao watetezi wapo katika hatari ya kuukosa uchampion wa ligi hiyo msimu ujao.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE