Duniani

Umewahi kufikiria itakuja kutokea Lexus ya mabox? Tayari imekamilika, hii hapa… +Pichaz & Video

on

Ni raha wakati mwingine kujua kwamba ukifikiri nje ya box na kufanya ubunifu mzuri hata Dunia inakutambua !!

Lexus ni gari ya kifahari sana, lakini ni gari ambazo zinafahamika pia… lakini eti kuna LEXUS ya maboksi?! Hiyo ni story nzuri kuijua mtu wangu !!

lexus1_3465325b

Hii ndio Lexus yenyewe ya maboksi !!

2014-Lexus-IS-350-fsport-exterior-beauty-overlay-1204x677-IS1345

Hii ndio LEXUS IS yenyewe halisi.

Kuna mchezo wa zamani hivi huwa wanacheza watoto, unakunja karatasi gumu linakuwa na umbo kama ndege, alafu unarusha hewani… lakini jamaa walichokifanya sio mchezo wa kitoto tena, ni kitu chenyewe kabisa.. Lexus imeundwa kwa maboksi mpaka mwisho alafu wakaiwasha na ikaingia mtaani kama gari ya ukweli kabisa.

Wataalam waliofanya hii kazi Uingereza wamesema mpaka matairi ya gari yameundwa kwa maboksi pia, kazi yote imeisha kwa muda wa miezi mitatu.

520509

Ili kupatikana tairi ilibidi vikatwe vipande vingi vya Boksi vyenye muundo huu na kuunganishwa kwa gundi.

Kazi imekwisha na gari linatembea japo halijapewa kibali kukatisha barabarani kama magari mengine.. mbali ya maboksi kitu kingine kilichoongezeka kwenye uundaji wa gari hilo ni chuma kizito ambacho kiko kwa chini ya gari pamoja na motor ambayo inafanya gari itembee, lakini maboksi pia yaliunganishwa kwa gundi ya maji ambayo inatokana na miti !!

340

Kiwanda kilichounda hii gari hata sio kikubwa, kazi kubwa imefanyika hapa.. ukiangalia unaona kabisa siti za Lexus pamoja na tairi zake zikiwa zimekamilika kabisa.

a03906c37d2e5ef962354dd074db1ebe

Ukifungua mlango upande wa Dereva kunaonekana hivi.

Cardboard-Origami-Car_Lexus_dezeen_936_14

Huu ndio muonekano wa dashboard ya gari… mshale wa mafuta na wa speed imechorwa tu kwa kalamu.

lexuscardboard8

lexus-cardboard-origami-car-07

Hapa ni katikati ya kiti cha dereva na abiria wa mbele, hiyo ni sehemu ya gia na vitu vingine.

lexus-full-sized-cardboard-origami-car-designboom-08-818x546

Lexus II

Lexus

Mchuma umekamilika namna hiyo mtu wangu.

Hii story nimeona niitafute na video yake kabisa, hii hapa na inaonekana kuanzia mwanzo jamaa wanavyoanza kutengeneza mpaka mwisho… Ubunifu wao ilikuwa kwa ajili ya kuionesha tu Dunia kwamba kuna gari inaweza kutengenezwa kwa njia hii nyingine mbali na ilivyozoeleka.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments