Beki wa kimataifa wa Ufaransa Patrice Evra ambaye amewahi kuitumikia klabu ya Manchester United ya Uingereza kwa kipindi cha miaka nane, October 14 amezungumzia uamuzi wa Man United kumuacha aondoke timu hiyo na kutimkia klabu ya Juventus ya Italia.
Patrice Evra ambaye amedumu katika klabu ya Manchester United kwa kipindi cha miaka nane, hakufurahishwa na uamuzi wa Man United kumuuza kwenda Juventus ya Italia kwa dau la pound milioni 1.5. Licha ya kushinda mataji kadhaa akiwa katika klabu yake mpya ya Juventus, Evra anasema uhamisho wa yeye kuondoka Man United ulilazimishwa na wala haukuwa uamuzi wake.
“Bado ni ngumu kuzungumzia kuondoka kwangu Man United lakini siku moja nitakapokuwa nimestaafu soka nitakuwa tayari kuzungumzia hili kwa kina. Nilikuja Turin kwa ajili ya familia yangu sababu Man United waliingiza kifungu ambacho kilibadili kila kitu, kitu ambacho kilinikera”>>> Evra
“Lakini sijutii uhamisho huu ambao mwisho wake umekuja kuwa na mrejesho zaidi ya chanya kwangu, najisikia furaha Serie A licha ya kuwa uhamisho huu ulikuwa wa bahati mbaya kuliko chaguo langu. Kwa sasa malengo yangu ni kuhakikisha nashinda mataji Juventus na timu yangu ya taifa ya Ufaransa”>>> Evra
Beki huyo wa zamani wa klabu ya Manchester United ya Uingereza, akiwa na Man United amecheza jumla ya mechi 379 na kutwaa mataji matano ya Ligi Kuu Uingereza, moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya na mataji mengine tisa hiyo ni kwa muda wa miaka nane aliyodumu katika klabu hiyo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.