Kuna idadi kubwa ya Majimbo Marekani wao hawana tatizo kabisa na masuala ya Bangi… imehalalishwa na inapatikana Madukani kama bidhaa nyingine za kawaida, sio nchi nyingi ambazo zimekubaliana kuhalalisha Bangi, Tanzania nayo imo.
Australia walianzisha Kampeni mwaka 2013 kuishawishi serikali ibadilishe Sheria ili kuhalalisha matumizi ya Bangi, majibu yaliyopatikana miaka miwili baadaye yani mwaka 2015 ni kwamba zaidi ya watu 246,000 wanahitaji Sheria irekebishwe na Bangi iruhusiwe kwa ajili ya kusaidia watu wenye matatizo na wanaohitaji Bangi kama tiba !!
Serikali ya Australia imeamua kulishughulikia hilo, kwa sasa wako kwenye mpango kuruhusu Bangi itumike kwa matumizi ya Matibabu, Sheria iliyopo kwa sasa hairuhusiwi kulima, kutumia au kukutwa na Bangi.. ukikamatwa ni kifungo au faini ambayo inatofautiana kutokana na Kanuni za Jimbo husika.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE