October 17 ndio siku ambayo Ligi Kuu soka Tanzania bara iliendelea kwa michezo kadhaa kupigwa katika viwanja tofauti tofauti, uwanja wa Taifa Dar Es Salaam ulipigwa mchezo ambao uliamua nani atapata nafasi ya kuongoza katika msimamo wa Ligi Kuu soka Tanzania bara.
Dar Es Salaam Young African walicheza dhidi ya Azam FC, mechi hii ilikuwa ni moja kati ya mechi za kuvutia, kwani Yanga na Azam FC zote zina point 15 kila mmoja na wote wamecheza jumla ya mechi 5 ila hii ilikuwa ni mechi ya sita kwa timu zote mbili. Kabla ya mechi kumalizika Yanga alikuwa anaongoza msimamo wa Ligi kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa, lakini mechi imemalizika kwa sare ya goli 1-1.
Kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika dakika ya 45 Donald Ngoma alipachika goli la kwanza baada ya kuitumia pasi safi kutoka kwa Juma Abdul, kipindi cha pili Azam FC walifanya mabadiliko kwa kumtoa Alan Wanga na kumuingiza Kipre Tchetche mshambuliaji ambaye alitumia vizuri pasi ya Farid Musa dakika ya 83 na kusawazisha goli. Licha ya Yanga kupata penati walishindwa kuitumia baada ya Kamusoko kupeleka mikononi mwa Aishi Manula,
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu October 17
- Maji Maji 1 – 0 African Sports
- Mbeya City 0 – 1 Simba
- Ndanda FC 0 – 0 Toto African
- Stand United 3 – 0 Tanzania Prisons
- Coastal Union 0 – 1 Mtibwa Sugar
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.