Tukiwa bado tuko kwenye headlines za Uchaguzi 2015 stori iliyochukua kasi katika vyombo vya habari pamoja na mitandao ni kuhusiana na wananchi kusimama mita 200 pale wanapomaliza kupiga kura siku ya tarehe 25, 2015, sasa mahakama Kuu Dar imesema hairuhusiwi watu kufanya mkusanyiko wowote hata nje ya umbali wa mita 200 baada ya kupiga Kura.
Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Tulia Ackson alisema…’Ni kwamba kifungu cha 104 kidogo cha kwanza kinakataza bila kujali umbali wake kutoka kwenye kituo cha kupigia kura ambacho baadae kinabadilika kina kuwa kituo cha kuhesabia kura, na la pili linalokatazwa katika lile jengwa ambapo kura zinahesabiwa mtu haruhusiwi kuvaa nembo au sare ya chama chochote kinachomuonesha yeye yupo upande fulani wa kisiasa’ – Tulia Ackson
‘Sasa la tatu ambalo pia kile kifungu kinakataza cha 104 kinakataza pia katika umbali wa mita 200 mtu yoyote asivae nembo au kuwa na picha yoyote ya chama au hata bendera yoyote kwenye umbali huo kwa hiyo hayo ndio mambo matatu yaliyokatwaza’ – Tulia Ackson
‘kama mtu hatofuata sheria basi adhabu yake ni Elfu 50 analipa lakini lile limeeleza kuwa ni kosa la jinai kwahiyo sio tu adhabu ya Elfu 50 mtu atalipa kirahisi hapana lazima akamatwa na kuwa chini ya vyombo vya sheria‘ – Tulia Ackson
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Tulia Ackson
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.