Good Morning mtu wangu, uchambuzi wa magazeti @CloudsFM The People’s Station umekupita? Jukumu langu kwako ni kuhakikisha zile zote kubwa za leo zinakufikia, baadhi zikiwa…
NEC imetangaza matokeo ya Urais kwenye majimbo 113 huku Dk. John Magufuli akiongoza kwenye majimbo mengi na Edward Lowassa kufuatia nyuma, umoja wa Ulaya EU wameipongeza Tanzania kwa kufanya Uchaguzi wa amani, Jaji Lubuva amesema hataki malumbano na Chama chochote cha Siasa wala ugomvi na wagombea wowote kwani NEC imetangaza matokeo bila upendeleo.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, LHRC imesikitishwa na kitendo cha wagombea kujitangazia matokeo kinyume na Sheria, UKAWA watawala Dar es salaam, wafanikiwa kushinda majimbo mengi wadai matokeo ya Urais yamechakachuliwa, Mzee Mrema asema pamoja na kushindwa kutetea jimbo la Vunjo kwa kupata Ubunge kitendo hicho sio mwisho wa yeye kujihusisha wala kushiriki kwenye siasa.
Jeshi la Polisi Tanzania wamewaonya wafuasi wa siasa nchini haswa vijana kuacha kushiriki kwenye vurugu zinazolenga kuvuruga au kuchelewesha matokeo kwenye maeneo mbalimbali haswa katika miji mikubwa kwani wakikamatwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Wakati NEC ikiendelea kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015, UKAWA wameendelea kupinga matokeo hayo wakidai yanachakachuliwa ili kumuwezesha mgombea nafasi Urais CCM kushinda, wasisitiza kuwa Tume inatakiwa kutangaza matokeo halali na kuacha upendeleo.
Unaweza kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast kwenye hii sauti hapa chini.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.