Hakika huu hauwezi kuwa msimu mbaya tu kwa kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho bali ni mwaka mbaya kwake, Jose Mourinho ambaye kikosi chake huwa akifanyi vizuri kwa mechi za hivi karibuni amekuwa akiingia katika headlines kutokana na kutofautiana na watu wanaomzunguuka kama waamuzi na daktari wa timu Eva Carneiro.
Usiku wa November 2 mtandao maarufu wa habari Uingereza express.co.uk uliandika maamuzi ya shirikisho la soka Uingereza FA baada ya kupatikana na hatia ya kosa la utovu wa nidhamu kwa kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho, kocha huyo amefungiwa mechi moja na FA na kutozwa faini ya pound 40,000 kwa kosa la utovu wa nidhamu alilolionesha katika mechi aliyopoteza dhidi ya West Ham United.
Kocha huyo wa Chelsea amekubali adhabu hiyo kutoka FA na atakosa mchezo dhidi ya Stoke City ugenini kutokana na kosa la kuwatolea maneno mabovu waamuzi wa mchezo dhidi ya West Ham United October 24 2015 tukio ambalo lilimfanya aondolewe na muamuzi katika benchi. Hata hivyo Chelsea wamepoteza jumla ya mechi sita katika mechi zao 11 walizocheza katika Ligi Kuu msimu huu. Mourinho alitenda kosa hilo wakati wa mapumziko ya mchezo huo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.