Uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita? Kama ulikuwa mbali na radio yako na hukuweza kuzipata zote kwenye kuperuzi na kudadis karibu ucheki na hizi nyingine hapa chini kufidia.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, TMA imewatahadharisha wananchi kuwa mvua kubwa za El Nino zinazosababishwa na ongezeko kubwa la joto zinategemea kunyesha kwa kasi mwezi wa November na December katika maeneo mbalimbali ikiwemo Dodoma, Mwanza, Mbeya, Njombe, Iringa, Kigoma, Katavi, Singida, Morogoro, Pwani na Dar es salaam.
Kamati kuu ya CCM imefuta matokeo ya kura za maoni katika jimbo la Handeni, Tanga ambako Omari Abdallah Kigoda alikuwa ameshinda, Nape Nnauye amesema kutokana na kufutwa kwa matokeo hayo, uchaguzi wa kura za maoni katika jimbo hilo unarudiwa leo, sababu kuu ya matokeo hayo kufutwa ni matokeo hayo kuonyesha kuwa hakuna mshindi aliyepata kura za kuridhisha kuingia katika ushindani na vyama vingine.
Wasomi na Wachambuzi wa masuala ya kisiasa kutokea Chuo Kikuu cha Dar es salaam wamesema Rais mteule Dk John Magufuli anakabiliwa na changamoto kuu nane baadhi zikiwa namna ya kutatua mgogoro wa kisiasa Zanzibar, Ongezeko ya deni la Taifa, changamoto ya mchakato wa Katiba mpya na upinzani wa kisiasa uliokomaa.
Alhamisi wiki hii Rais Mteule Dk John Magufuli ataapishwa kuwa Rais wa Tanzania na mara baada ya hapo kuanza kutekeleza ahadi zake huku kipimo chake cha kwanza kitakua kutimiza ahadi yake ya kuunda Baraza dogo la Mawaziri lenye sifa kubwa ya utendaji kazi.
Aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje akanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Mwanza, Wenje amesema taarifa hizo sio za kweli, yupo salama na kwa sasa yupo nchini Namibia kwa shughuli za kichama.
Unaweza kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast hapa chini kwenye hii sauti.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.