Ni siku moja baada ya Rais Magufuli kukabidhiwa kiti cha Urais ameanza kazi yake kwa surprise, Rais JPM amekatisha kwa mguu kutoka Ikulu mpaka Wizara wa Fedha maeneo ya Posta na kukuta ndani ya Ofisi kuna wafanyakazi ambao hawapo Ofisini na ilikuwa ni muda wa kazi.
ripota wa millardayo.com alikutana na shuhuda akielezea namna alivyotembelea kutoka Ikulu mpaka kuingia Wizara ya fedha..’Mimi niliona watu walikuwa wanakimbia kumbe alikuwa ni rais wa awamo ya tano ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Joseph Magufuli anatembea kutokea Ikulu akielekea Wizara ya Fedha au hazina alikuwa na walinzi pamoja na magari yake yalikuwa yakitembelea’ – Shuhuda
‘Baada ya kutoka wizara ya fedha basi akaingia kwenye gari, mimi hii ni mara yangu ya kwanza kuona kiongozi kama huyu ameapishwa jana na leo ameanza kufanya kazi basi atakuwa kweli ni Rais wa tofauti kabisa’ – Shuhuda
Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Shuhuda akieleza jinsi Rais JPM alivyoingia wizara ya Fedha
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram naYouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.